Ongoza ya Bin Dohri, Hadhaarim wa Diaspora.- Poem by Abdallah Bin Eifan

Ninalirusha kombora, za salamu na za kheri,
Lizunguke Makadara, lifike hapo Bamburi,
Limkabidhi bendera, Kiongozi Bin Dohri,
Ongoza ya Bin Dohri, Hadhaarim wa Diaspora.

Hadhaarim wa Diaspora, wanangojea habari,
Ingawa tunakukera, vumilia usubiri,
Thawabu zako akhera, kwa Mola wetu Qahari,
Ongoza ya Bin Dohri, Hadhaarim wa Diaspora.

Nenda na wewe imara, kwa vyote uwe tayari,
Waeleze kwa busara, wape maneno mazuri,
Hatutaki masikhara, katiba iwe dhahiri,
Ongoza ya Bin Dohri, Hadhaarim wa Diaspora.

Diaspora Afrika, tunao watu hodari,
University wamefika, tunao maprofessori,
Na wengi wamesifika, wamekuwa mashuhuri,
Ongoza ya Bin Dohri, Hadhaarim wa Diaspora.

Diaspora Afrika, tunao na mawaziri,
Vizuri tumejiweka, tunao na matajiri,
Na wasomi kadhalika, wapo kama utitiri,
Ongoza ya Bin Dohri, Hadhaarim wa Diaspora.

Pigania zetu haki, tuwe mbele ya msitari,
Na haki ya kumiliki, ardhi na utajiri,
Nyuma katu tusibaki, tuwe kwenye mashauri,
Ongoza ya Bin Dohri, Hadhaarim wa Diaspora.
Tuwe kwenye serikali, kwa nguvu na kwa khiari,
Tuwepo kila pahali, huku tukitahadhari,
Pia vyeo mbalimbali, kututenga ni hatari,
Ongoza ya Bin Dohri, Hadhaarim wa Diaspora.

Umoja tunautaka, peke yetu wa Kusini,
Hatutaki takataka, wajinga wa Kaskazini,
Kunyamaza tumechoka, kuishi na mashetani,
Ongoza ya Bin Dohri, Hadhaarim wa Diaspora.

Kuchagua mabalozi, hapa kwetu tuchaguwe,
Tunao wenye ujuzi, watoto wetu wenyewe,
Hatutaki ubaguzi, Bungeni tuchaguliwe,
Ongoza ya Bin Dohri, Hadhaarim wa Diaspora.

Na masomo kadhalika, scholarships tupewe,
Kwa watoto Afrika, watuletee tuzigawe,
Beti kumi nimefika, ninawaaga kwa shangwe.
Ongoza ya Bin Dohri, Hadhaarim wa Diaspora.

Abdallah Bin Eifan
Jeddah.

Post a Comment

0 Comments